CGP. KATUNGU AAGIZA KUONGEZA KASI UJENZI WA GEREZA JIPYA


 

Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP. Jeremiah Yoram Katungu, amewataka wataalamu wa ujenzi wa Jeshi la Magereza wanao simamia ujenzi wa mradi wa Gereza jipya la Msalato, kuongeza kasi ili mradi huo ukamilike kwa wakati.


CGP. Katungu ametoa agizo hilo leo, Agosti 28, 2026, alipotembelea na kukagua mradi huo uliopo eneo la Msalato jijini Dodoma.


Aidha, amewapongeza wataalamu wote wanaotekeleza mradi huo kwa uwajibikaji wao huku akisisitiza umuhimu wa mradi huo kutumika kama sehemu ya mafunzo ya kuwarekebishaji kwa wafungwa.


Pamoja na mambo mengine CGP Katungu, ameawaagiza wataalamu hao kuhakikisha wanawashirikisha  wafungwa katika ujenzi kama sehemu ya stadi za kazi kwa  kuzingatia Sheria, Kanuni na  Taratibu za urekebishaji ili iwe sehemu ya kuwaandaa pindi  watakapomaliza vifungo vyao waweze kujitegemea kiuchumi kwaajili yao , familia zao na kwa taifa kwa ujumla.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Popular Items